Waziri Mkuu aweka jiwe la msingi jengo la ‘Viwango House’

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa leo Juni 4 ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa jengo la Shirika la Viwango Tanzania (TBS) ‘Viwango Hause’ katika hafla iliyofanyika kwenye viwanja vya Ofisi hiyo Njedengwa, jijini Dodoma. Akizungumza katika hafla hiyo, Majaliwa amesema kuwa Serikali ya awamu ya sita inatambua kuwa viwango vya ubora si tu vinahusiana na …
WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa leo Juni 4 ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa jengo la Shirika la Viwango Tanzania (TBS) ‘Viwango Hause’ katika hafla iliyofanyika kwenye viwanja vya Ofisi hiyo Njedengwa, jijini Dodoma.
Akizungumza katika hafla hiyo, Majaliwa amesema kuwa Serikali ya awamu ya sita inatambua kuwa viwango vya ubora si tu vinahusiana na bidhaa bora, bali pia vinaimarisha afya na uchumi wa nchi.
Amesema viwanda vinapaswa kuzalisha bidhaa ambazo zinaweza kununulika hata nje ya nchi.
“Tunataka mataifa mengine yakimbilie bidhaa zetu,” amesema Majaliwa.
Ujenzi wa jengo hilo ambao umefikia asilimia 76 unatarajiwa kugharimu shs bilioni 25.3 ikijumuisha kodi ya ongezeko la thamani na gharama za mshauri elekezi.
Jengo hilo linatarajiwa kukamilika Agosti 30, 2025.