Wasaini mkabata kuongeza mbinu za ufaulu kwa wanafunzi

ARUSHA: TAASISI ya Elimu Tanzania (TET) kwa kushirikiana na Kampuni ya Simu ‘Vodacom’ na Taasisi ya Twaweza wamesaini mkataba wa makubaliano kuwezesha walimu kutoa mbinu kwa wanafunzi kwa ajili ya kuwezesha ongezeko la ufaulu shuleni. Akisaini makubaliano hayo, Mkurugenzi wa Idara ya Ubunifu na Uboreshaji Mitaala, Angela Katabazi kwa niaba ya Mkurugenzi wa TET Dk, …
ARUSHA: TAASISI ya Elimu Tanzania (TET) kwa kushirikiana na Kampuni ya Simu ‘Vodacom’ na Taasisi ya Twaweza wamesaini mkataba wa makubaliano kuwezesha walimu kutoa mbinu kwa wanafunzi kwa ajili ya kuwezesha ongezeko la ufaulu shuleni.
Akisaini makubaliano hayo, Mkurugenzi wa Idara ya Ubunifu na Uboreshaji Mitaala, Angela Katabazi kwa niaba ya Mkurugenzi wa TET Dk, Aneth Komba, ameshukuru ushirikiano huo unaowezesha wanafunzi kupata mbinu za kujifunza na kufaulu zaidi na kusisitiza kuwa serikali itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali katika kuhakikisha sekta ya elimu inakua zaidi.
Naye, Anastazia Rugaba ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Utetezi katika Taasisi ya Twaweza amesema Lupita mradi wa kiufunza ambayo ni motisha ya ustadi kwa walimu ili kuwezesha ufaulu ambapo kupitia Taasisi ya Vodacom imewezesha kufikia shule za msingi 865 wa darasa la kwanza hadi la tatu lengo ni kufikia wanafunzi 360,000
Wakati huo huo, Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania, Foundation,Zuweina Farah amesema kampuni hiyo itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali kuinua sekta ya elimu nchini ili kuwezesha watoto kujiua kusoma kuandika na kuhesabu katika kuinua kiwango cha ufaulu nchini.
“Tunatoa motisha ndogo ya pesa kwa waalimu kwa kila ustadi ambao huwapatia wanafunzi, kimsingi katika ustadi wa kusoma na hesabu katika darasa, moja, ngazi mbili na tatu, kwa hivyo ustadi zaidi ambao mwanafunzi wa masomo, pesa zaidi ambayo mwalimu anapata”