Wanawake Pwani wahamasishwa kushiriki uchaguzi

PWANI: Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT)wa Chama Cha Mapinduzi Tanzania (CCM), Mary Chatanda Amewasihi wananchi hususani Wanawake kujitokeza kwa wingi kwenye zoezi la upigaji kura kwenye Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Mwezi Oktoba Mwaka Huu. Lengo likiwa ni kutimiza haki yao kikatiba na kuwachagua Viongozi watakaochagiza Juhudi zinazofanywa naserikari ya Awamu ya Sita …
PWANI: Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT)wa Chama Cha Mapinduzi Tanzania (CCM), Mary Chatanda Amewasihi wananchi hususani Wanawake kujitokeza kwa wingi kwenye zoezi la upigaji kura kwenye Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Mwezi Oktoba Mwaka Huu.
Lengo likiwa ni kutimiza haki yao kikatiba na kuwachagua Viongozi watakaochagiza Juhudi zinazofanywa naserikari ya Awamu ya Sita kwa kuwaletea Maendeleo kwenye Maeneo yao.
Chatanda ameelza hayo leo wilayani Mkuranga mkoani Pwani akiwa katika ziara yake ambayo ameambatana na Makamu Mwenyekiti wa UWT, Zainab Khamis Shomari pamoja na wajumbe wa kamati tendaji na wajumbe wa baraza kuu wa jumuiya hiyo.
Katika ziara hiyo Chatanda na wajumbe wake wamekagua utekelezaji wa Ilani ya CCM ya Mwaka 2020/25 kuhakikisha imetekelezwa ipasavyo na watendaji wa serikali kwani Rais Samia Suluhu Hassan ametoa fedha nyingi kwa ajili ya maendeleo mkoani humo.
Chatanda amesema kwenye mkutano mkuu wa CCM walimteua Mwenyekiti wa chama hicho kuwa mgombea Urais katika uchaguzi mwaka huu na Katibu Mkuu, Balozi Dk Emmanuel Nchimbi kuwa mgombea mwenza katika uchaguzi huo.
Amesisitiza katika mkutano wa mwisho wamezindua ilani ya uchaguzi ya 2025/2030 na wameipokea na kuendelea kuinadi ili wananchi wawese kujua ni nini kitatekelezwa katika kioindi hicho cha miaka 5 akiwasisitiza kushiriki uchaguzi ili kuoata viongozi watakaoitekeleza ilani hiyo.
Kwa upande wake Shomari amewasisitiza wananchi wa Mkuranga na Tanzania kwa ujumla kujenga na kuimarisha umoja upendo na mshikamano hususani kinaposfika kipindi cha kura za maoni kwa kutokuruhusu kusababisha mpasuko na mfarakano kati yao.
Akitoa taarifa ya utekelezaji wa ilani katika wikaya hiyo Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Hadija Nassir jumla ya miradi 39 yenye thamani ya Zaidi ya Sh bilioni 500 ambayo itakaguliwa wilayani hapo na kutolewa taarifa ya utekelezaji wake kwa Mwenyekiti wa CCM Taifa ambaye ni Dk Samia.