Wabunge wapitisha bajeti Wizara ya Afya

DODOMA; WABUNGE leo Juni 3, 2025 wamepitisha bajeti ya Wizara ya Afya yenye makadirio ya Sh 1,618,191,235,000.00, ili kuweza kutekeleza malengo na vipaumbele iliyojiwekea kwa mwaka 2025/26. Jana Waziri wa Afya Jenista Mhagama, aliwasilisha bungeni hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya fedha ya Wizara ya Afya kwa mwaka 2025/2026, ikiwa na vipaumbele 10. …
DODOMA; WABUNGE leo Juni 3, 2025 wamepitisha bajeti ya Wizara ya Afya yenye makadirio ya Sh 1,618,191,235,000.00, ili kuweza kutekeleza malengo na vipaumbele iliyojiwekea kwa mwaka 2025/26.
Jana Waziri wa Afya Jenista Mhagama, aliwasilisha bungeni hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya fedha ya Wizara ya Afya kwa mwaka 2025/2026, ikiwa na vipaumbele 10.
Baadhi ya vipaumbele hivyo ni kuimarisha huduma za kinga dhidi ya magonjwa ya kuambukiza yakiwemo magonjwa milipuko, magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele, magonjwa yasiyoambukiza na huduma za Lishe.
Vipaumbele vingine ni kuimarisha upatikanaji na ubora wa huduma za afya zinazotolewa katika ngazi zote kuanzia Zahanati hadi Taifa; Kuimarisha mifumo ya ugharamiaji wa huduma za afya nchini ikiwa ni pamoja na kuendelea na utekelezaji wa Sheria ya Bima ya Afya kwa Wote.
–