Viti kusaidia huduma afya kinywa na meno

DAR ES SALAAM: HUDUMA ya afya ya kinywa na meno nchini imeendelea kuimarika katika maeneo mbalimbali baada ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) kupokea mashine mbili za huduma hiyo kutoka kwa Taasisi ya Foshan DYM Medical Instrument CO.,LTD ya China. Akizungumza leo Juni 4, 2025 jijini Dar es Salaam, Ferdinand Machibya, …
DAR ES SALAAM: HUDUMA ya afya ya kinywa na meno nchini imeendelea kuimarika katika maeneo mbalimbali baada ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) kupokea mashine mbili za huduma hiyo kutoka kwa Taasisi ya Foshan DYM Medical Instrument CO.,LTD ya China.
Akizungumza leo Juni 4, 2025 jijini Dar es Salaam, Ferdinand Machibya, Mkuu wa Skuli ya Afya ya Kinywa na Meno kutoka MUHAS amesema taasisi ya afya ya kinywa na meno Muhimbili inaongoza kwa mafunzo na kutoa wataalamu wa huduma hiyo, hivyo wanahitaji usaidizi zaidi wa vifaa vya huduma hiyo.
“Viti hivi vina kiwango cha juu sana, kina kamera ambayo mgonjwa unaweza ukamuonesha kuna tatizo gani kwenye kinywa, lakini kuna sensa ambayo ukipitisha mkono unazima na kuwasha taa,” amesema Machibya.
SOMA ZAIDI
MUHAS waja na mpango wa mazoezi usimamizi kitabibu
Amesema ongezeko la vifaa vya aina hiyo vitawezesha kutoa mafunzo kwa watu wengi na kupanua wigo wa huduma ya kinywa na meno. Amesema mahitaji ni makubwa na wanahitaji viti visivyopungua 100 ili kuendelea kuimarisha zaidi huduma.
Bonnie Hong, kutoka Taasisi ya Foshan DYM Medical Instrument CO.,LTD amesema wataendelea kushirikiana an MUHAS kuboresha huduma ya afya ya kinywa na meno.
“Ni heshima kubwa kuwasilisha viti hivi, ni dhamira yetu kuwa vitawezesha kutoa mafunzo zaidi,” amesema Boniie Hong.
Daktari wa magonjwa ya kinywa na meno, Suzana Sabasaba amesema viti hivyo vitawezesha wanafunzi kupata mafunzo na kutoa huduma bora kwa wananchi.