Vijana watakiwa kuonesha vipaji vyao

Habari Leo
Published: Jun 08, 2025 06:46:56 EAT   |  Entertainment

SHINYANGA: VIJANA wameshauriwa kujitokeza kuonyesha vipaji vyao kwenye maonesho mbalimbali ili wapate kusaidiwa katika ajira na kujiajiri wenyewe. Hayo yamesemwa leo na Kiongozi Mkuu wa Kimkakati wa Chapa ya Jambo group na Jambo Media, Nickson George kwenye uzinduzi wa kinywaji cha Jambo mwamba challenge kilichozinduliwa na msanii wa Singeli nchini Dvoice kutoka WCB iliyopo. George …

SHINYANGA: VIJANA wameshauriwa kujitokeza kuonyesha vipaji vyao kwenye maonesho mbalimbali ili wapate kusaidiwa katika ajira na kujiajiri wenyewe.

Hayo yamesemwa leo na Kiongozi Mkuu wa Kimkakati wa Chapa ya Jambo group na Jambo Media, Nickson George kwenye uzinduzi wa kinywaji cha Jambo mwamba challenge kilichozinduliwa na msanii wa Singeli nchini Dvoice kutoka WCB iliyopo.

George amewaeleza vijana kuwa mtaji wa kwanza ni uwezo binafsi ambao utawafanya kuwatoa sehemu moja kwenda nyingine wasikae nyumbani kusubiri kuajiriwa watoke kwenye majukwaa kama haya ili waweze kuonekana.

“Mzazi ampende mwanaye asimuzuie amwambie kijana wake kuwa ni mwamba ajitokeze kwenye kipaji alichonacho asimkatishe tama wapo waliotumia vipaji binafsi hivi sasa ni matajiri,”amesema George.

George amesema asilimia 70 ni vijana hivyo ameishauri serikali kuwa na majukwaa kama hayo ili waoneshe vipaji vyao kwani wapo wengi ni mwamba katika ushindi kupitia michezo kama vile kuruka kamba,kukimbia,kudansi,kupiga danadana na leo lebo ya mwamba imewekwa kwenye vinywaji kwaajili ya kuhamasisha vipaji.

Uzinduzi wa Jambo mwamba challenge au mimi ni Mwamba Challenge ulimfanya Dvoice kupiga pushapu 20 huku kiongozi mkuu wa chapa ya Jambo Nickson George akipiga pushapu 60 sambamba na vijana kujitokeza katika mashindano ya kula,kucheza kuvuta kamba na kupiga danadana mpira kwa miguu.