‘Tutapambana kuhakikisha mifumo hospitali isomane’

WAZIRI wa Afya Jenista Mhagama, amesema wizara yake itapambana kuhakikisha mifumo ya vipimo vinavyofanywa kwa wagonjwa visomane katika hospitali zote nchini. – Akifanya majumuisho kwenye hoja mbalimbali za wabunge waliochangia hotuba yake ya makadirio ya mapato na matumizi ya fedha ya Wizara ya Afya kwa mwaka 2025/2026, Waziri Mhagama amesema tayari wameanza na baadhi ya …
WAZIRI wa Afya Jenista Mhagama, amesema wizara yake itapambana kuhakikisha mifumo ya vipimo vinavyofanywa kwa wagonjwa visomane katika hospitali zote nchini.
–
Akifanya majumuisho kwenye hoja mbalimbali za wabunge waliochangia hotuba yake ya makadirio ya mapato na matumizi ya fedha ya Wizara ya Afya kwa mwaka 2025/2026, Waziri Mhagama amesema tayari wameanza na baadhi ya hospitali za Rufani za Mikoa na za Kanda na sasa wanaelekeza nguvu kwenye hospitali nyingine za chini.
–
Amesema haiwezekani mgonjwa anatoka Songea amepimwa, lakini akifika Njombe atatakiwa kupimwa upya kipimo kilekile na wakati mwingine kumuongezea gharama mgonjwa.
–