‘Treni ikifika Dodoma saa 1;30 asubuhi itasaidia kukuza uchumi’

Habari Leo
Published: Jun 05, 2025 07:31:52 EAT   |  News

DODOMA; NAIBU Spika Mussa Azzan ‘Zungu’, amesema kama Shirika la Reli nchini (TRC), litabadilisha ratiba za safari zake ya treni ya SGR kutoka Dar es Salaam ikafika Dodoma saa 1;30 asubuhi na pia ya kutoka Dodoma ikafika saa 1;30 asubuhi itasaidia sana kukuza uchumi. Ametoa kauli hiyo leo muda mfupi baada ya Waziri Mkuu, Kassim …

DODOMA; NAIBU Spika Mussa Azzan ‘Zungu’, amesema kama Shirika la Reli nchini (TRC), litabadilisha ratiba za safari zake ya treni ya SGR kutoka Dar es Salaam ikafika Dodoma saa 1;30 asubuhi na pia ya kutoka Dodoma ikafika saa 1;30 asubuhi itasaidia sana kukuza uchumi.

Ametoa kauli hiyo leo muda mfupi baada ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kumaliza kujibu maswali ya wabunge, ambapo miongoni mwa maswali hayo lipo lililoulizwa na Mbunge wa Viti Maalumu, Asha Abdallah Juma aliyehoji mikakati ya serikali kuongeza safari za SGR.

Naibu Spika amesema juzi alikuwa anazungumza na kiongozi mmoja wa TRC akamwambia wana mpango wa kuleta teni itakayotumia muda wa saa 2;45 kati ya Dar es Salaam na Dodoma na kueleza kuwa hilo ni jambo la kupongezwa sana kwa Serikali ya Rais Dk Samia Suluhu Hassan.

“Lakini nikuombe Mheshimiwa Waziri Mkuu kama wataweza kubadilisha ratiba treni zao ziingie Dodoma saa 1;30 asubuhi na ikitoka hapa iingie Dar es Salaam saa 1;30 asubuhi itasaidia sana kukuza uchumi na kuhakikisha viongozi wa serikari, wabunge, watumishi wanawahi shughuli za kiserikali kwa muda unaotakiwa,” amesema Naibu Spika.