TBS yanogesha mambo ujenzi maabara Dodoma, Mwanza

Habari Leo
Published: Jun 03, 2025 11:17:52 EAT   |  News

DODOMA; Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Dk Ashura Katunzi amesema katika kutekeleza azma ya Serikali kuhakikisha wananchi wanapata huduma kwa ukaribu na kupunguza gharama, shirika hilo linaendekea na  ujenzi wa maabara za kisasa katika mikoa ya kimkakati ya Dodoma, Mwanza na baadaye Arusha. Dk Katunzi amesema hayo leo Juni 3, 2025 akizungumzia …

DODOMA; Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Dk Ashura Katunzi amesema katika kutekeleza azma ya Serikali kuhakikisha wananchi wanapata huduma kwa ukaribu na kupunguza gharama, shirika hilo linaendekea na  ujenzi wa maabara za kisasa katika mikoa ya kimkakati ya Dodoma, Mwanza na baadaye Arusha.

Dk Katunzi amesema hayo leo Juni 3, 2025 akizungumzia uwekeji wa  jiwe la msingi katika jengo la TBS la kimkakati ambalo litagharimu Sh bilioni 25 na jiwe la msingi litawekwa kesho na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

Amesema shirika linaendelea na ujenzi katika Jiji la Dodoma, Mwanza na kuwa mkakati ujao ni kujenga pia Jiji la Arusha.

Dk Katunzi amesema  ghorofa tatu katika jengo hilo litakuwa na maabara za kisasa za kiwango cha kimataifa zenye ithibati ya kimataifa ambazo ni za chakula, kemia na nguo na zitahudumia mikoa mitatu ya Kanda ya Kati ambayo ni Dodoma, Singida na Tabora pamoja na mikoa mingine ya jirani.

“Kwa sasa ujenzi wa jengo hili umefikia asilimia 75 ambalo litaendelea kuongeza thamani kwa maana Watanzania tutakaowahudumia.”

“Maabara hizo zikiwepo Dodoma itasaidia kuongeza ufanisi katika ufanyaji kazi wetu tunaowahudumia kwa sasa maabara zetu ziko Dar es Salaam ili kufanya maamuzi ya ubora na usalama, maabara Dodoma itatusaidia kutoa maamuzi ya haraka na kuwahudumia kwa haraka. Hii pia itapunguza msongamno wa sampuli kupeleka Dar es Salaam.”

“ Ujenzi wa maabara utasaidia kusogeza huduma karibu na wananchi na kuongeza ufanisi katika utoaji wa majibu ya vipimo vya sampuli,” amesema.