Taasisi zatakiwa kujitathmini

ARUSHA: AZAKI na taasisi zisizo za kiserikali zimetakiwa kujitathmini kama zipo njia panda au la katika kutekeleza majukumu yao kwa kila siku ya kiutendaji ikiwemo kuwaletea wananchi maendeleo Rais wa Taasisi ya Foundation For Civil Society (FCF) Dk, Stigmata Tenga ameeleza hay oleo wakati akizungumza na washiriki wa azaki ambao kwa pamoja wanajadili mambo mbalimbali …
ARUSHA: AZAKI na taasisi zisizo za kiserikali zimetakiwa kujitathmini kama zipo njia panda au la katika kutekeleza majukumu yao kwa kila siku ya kiutendaji ikiwemo kuwaletea wananchi maendeleo
Rais wa Taasisi ya Foundation For Civil Society (FCF) Dk, Stigmata Tenga ameeleza hay oleo wakati akizungumza na washiriki wa azaki ambao kwa pamoja wanajadili mambo mbalimbali kuhusu muhtakabali wa Azaki katika kuleta tija kwa nchi, wananchi na mikakati ya kwenda mbele zaidi ili kuhakikisha wananchi wanapata maendeleo.
Dk Tenga amesema katika kusherehekea miaka saba ya Azaki lazima pia wajitathimini kwenye mambo mbalimbali ikiwemo kujikwamua kiuchumi, ikiwemo fedha wanazozipata kwa wafadhili badala ya kupelekwa katika maeneo walitokusudia wanajikuta wanalazimika kulipia kodi Amazon zipo kwenye mifumo mingi.
“Mifumo mingi ya kodi nchini inarudisha nyuma maendeleo, sababu fedha tunazopata za wadau wa maendeleo tunalazimika kulipia kodi badala ya kwenda kufanya kazi zilizokusudiwa kwanwalengwa, ”
Amesisitiza ili azaki ziweze kusonga mbele zaidi zinapaswa kujitathimini katika mambo mbalimbali ikiwemo mabadiliko ya kidunia, utoaji huduma kwa wadau wa maendeleo sanjari na kupaza sauti pale wanapoona inafaa hususan katika maendeleo na haki za binadamu lakini pia watu wenye ulemavu wasibaguliwe na makundi maalum yawezeshwe ili kuhakikisha maendeleo yanafika kwa kila m wananchi.
Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Azaki (CSO) , CPA Mercy Silla amesisitiza azaki hizo kuendelea kuchagiza maendeleo ikiwemo kusaidia serikali kutatua changamotoz zilizopo na kuibua nyinginezo katika kuhakikisha maendeleo yanakua zaidi.