Sheria Bima ya Afya kwa wote kuanza 2025/26

DODOMA; WAZIRI wa Afya Jenista Mhagama, amesema utekelezaji wa Sheria ya Bima ya Afya kwa wote utaanza kwenye bajeti ya mwaka 2025/26 na kwamba itakuja na vifurushi vyake. Akifanya majumuisho kwenye hoja mbalimbali za wabunge waliochangia hotuba yake ya makadirio ya mapato na matumizi ya fedha ya Wizara ya Afya kwa mwaka 2025/2026, Waziri Mhagama …
DODOMA; WAZIRI wa Afya Jenista Mhagama, amesema utekelezaji wa Sheria ya Bima ya Afya kwa wote utaanza kwenye bajeti ya mwaka 2025/26 na kwamba itakuja na vifurushi vyake.
Akifanya majumuisho kwenye hoja mbalimbali za wabunge waliochangia hotuba yake ya makadirio ya mapato na matumizi ya fedha ya Wizara ya Afya kwa mwaka 2025/2026, Waziri Mhagama amesema amechukua hoja mbalimbali za wabunge kuhusu masuala ya bima ya afya na kuahidi kuwa nyingi zitajibiwa na sheria hiyo itakapoanza.