Rais Samia atembelea mradi nishati safi Sekondari Simiyu

Habari Leo
Published: Jun 16, 2025 17:41:32 EAT   |  News

DAR ES SALAAM: Rais Samia Suluhu Hassan ametembelea mradi wa nishati safi ya kupikia wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Simiyu iliyopo Bariadi mkoani Simiyu. Mradi huo unahusisha usimikaji wa mfumo wa kupikia kwa kutumia gesi yaani LPG, ikiwa ni sehemu ya jitihada za kupunguza utegemezi wa kuni na mkaa, hivyo kuchangia katika utunzaji wa …

DAR ES SALAAM: Rais Samia Suluhu Hassan ametembelea mradi wa nishati safi ya kupikia wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Simiyu iliyopo Bariadi mkoani Simiyu.

Mradi huo unahusisha usimikaji wa mfumo wa kupikia kwa kutumia gesi yaani LPG, ikiwa ni sehemu ya jitihada za kupunguza utegemezi wa kuni na mkaa, hivyo kuchangia katika utunzaji wa mazingira na kulinda afya ya wanafunzi na walimu.

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) imetoa ufadhili wa kiasi cha Sh milioni 14 kwa ajili ya ujenzi na usimikaji wa miundombinu ya nishati safi ya kupikia katika shule hiyo.