Mwanaharakati Rose Njeri ashtakiwa kukwamisha mtandao wa Bunge

Taifa Leo
Published: Jun 03, 2025 10:47:28 EAT   |  News

MWANAHARAKATI Rose Njeri ameshtakiwa kukwamisha mtandao wa Bunge na kusababisha shughuli za kamati ya Bunge kuhusu Fedha kutatizika. Kulingana na hati ya mashtaka alipofikishwa mahakamani Jumanne Juni 3, 2025, Bi Njeri anadaiwa kuunda programu iliyotuma baruapepe nyingi kuhusu Mswada wa Fedha na kusababisha mrundikano mkubwa. Bi Njeri amekuwa akizuiliwa na polisi tangu wiki jana, huku ripoti zikisema amekuwa akihamishwahamishwa kutoka kituo kimoja hadi kingine wakati wa wikendi ndefu ya Madaraka Day. Kumekuwa pia na hofu kuhusu hali yake ya kiafya huku familia yake ikisema ameugua maradhi ya ukosefu wa damu akiwa kizuizini. Akimwakilisha mshtakiwa, Wakili wa Cheo cha Juu aliye pia Kinara wa Wiper Kalonzo Musyoka alipinga Bi Njeri kujibu mashtaka akisema mashtaka hayo hayana mashiko kwa sababu mtandao unaodaiwa kujazwa uliundwa na Bunge kwa ajili ya kupokea maoni kutoka kwa umma kuhusu Mswada wa Fedha 2025. Habari zaidi ni kadiri tunavyozipokea… .