Mfumo kidigiti kudhibiti ubora wa shule

Habari Leo
Published: Jun 04, 2025 07:41:47 EAT   |  Educational

ARUSHA: SERIKALI imeanzisha mfumo wa kidigiti wa udhibiti ubora wa shule kwa viongozi wa elimu ili kuongeza ufanisi, uwazi, uwajibikaji na kuimarisha ukusanyaji, uchambuzi na utoaji wa mrejesho wa tathmini za shule kwa wizara na wadau wa elimu. Aidha, mfumo huo pia utawezesha utunzaji na uchakataji wa taarifa kwa urahisi na kwa wakati hivyo ni …

ARUSHA: SERIKALI imeanzisha mfumo wa kidigiti wa udhibiti ubora wa shule kwa viongozi wa elimu ili kuongeza ufanisi, uwazi, uwajibikaji na kuimarisha ukusanyaji, uchambuzi na utoaji wa mrejesho wa tathmini za shule kwa wizara na wadau wa elimu.

Aidha, mfumo huo pia utawezesha utunzaji na uchakataji wa taarifa kwa urahisi na kwa wakati hivyo ni vema kila mtu atoke na mpango mkakati wa kuboresha utendaji kazi

Hayo yamesemwa jijini Arusha na Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Carolyne Nombo wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya matumizi ya mfumo wa kidigitali wa Udhibiti Ubora wa Shule kwa Viongozi wa Elimu ngazi ya Mkoa, Halmashauri na Maofisa Udhibiti Ubora wa Shule na Tehama.

Amesema serikali itaendelea kuweka msukumo zaidi kwa watalaamu wabobezi wa mifumo ya Tehama ili kuhakikisha wanaleta tija zaidi katika kuleta mabadiliko kwenye sekta ya kidigitili kwani mafunzo hayo ni muhimu katila uboreshaji wa utendaji kazi kwa maofisa elimu ikiwemo uboreshaji wa elimu nchini.

Tanzania yaelezea uzoefu wake wa kidijiti Uswisi

“Ninaimani umahiri utaongezeka zaidi katika kuhakikisha matumizi sahihi ya mfumo wa kidigiti wa uthibiti ubora yanakua zaidi ili kuboresha utendaji na kuimarisha mbinu anuani na lazima mjue mafunzo hayo gharama yake Sh bilioni 1.2 katika mikoa yote nchini”

“Sasa hivi dunia ipo kidigiti ili mifumo hii iweze kufanya kazi kwa ufanisi lakini pia mtafundishwa wengine mbinu za kuwezesha wengine katika utendaji kazi ili kuleta tija kwa wadau wengine kulingana na sera ya elimu na mafunzo ikiwemo kihunzi cha zana zaidi ufundishaji katika kutekeleza vipaumbele katika uwazi na kuimarisha uwajibikaji”

Naye Mkurugenzi wa Uthibiti Ubora wa Shule kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Ephraim Simbeye, amesema mfumo wa kidigiti wa udhibiti ubora wa shule utarahisisha utendaji kazi na upatikanaji wa taarifa sahihi kwa wakati.