Mbunge ahoji mkakati afya bure kama ilivyo elimu

Habari Leo
Published: Jun 03, 2025 08:31:03 EAT   |  News

DODOMA; MBUNGE wa Donge, Soud Mohammed Jumah, amehoji bungeni, serikali ina  mkakati gani kuweka huduma za afya bure kama ilivyo katika elimu ya msingi na sekondari. Akijibu swali hilo bungeni leo, Naibu Waziri wa Afya, Dk Godwin Mollel, amesma serikali inaendelea kuboresha mifumo ya ugharamiaji wa huduma za afya kwa wananchi wasio na uwezo. “Tangu …

DODOMA; MBUNGE wa Donge, Soud Mohammed Jumah, amehoji bungeni, serikali ina  mkakati gani kuweka huduma za afya bure kama ilivyo katika elimu ya msingi na sekondari.

Akijibu swali hilo bungeni leo, Naibu Waziri wa Afya, Dk Godwin Mollel, amesma serikali inaendelea kuboresha mifumo ya ugharamiaji wa huduma za afya kwa wananchi wasio na uwezo.

“Tangu mwaka 1995, serikali imekua ikitekeleza sera ya msamaha wa gharama za matibabu kwa wananchi wasio na uwezo.

“Hata hivyo, kutokana na changamoto ambazo zimeendelea kujitokeza katika utekelezaji, serikali iko katika hatua za utekelezaji wa Sheria ya Bima ya Afya kwa Wote.

“Sheria hiyo itatoa fursa kwa watu wasio na uwezo kughramiwa bima ya afya na Serikali ili kuwawezesha kupata huduma za afya bila kikwazo cha fedha,” amesema Naibu Waziri.