Matawi sita ufufuo na uzima yafungiwa Mbeya

MBEYA: JESHI la Polisi mkoani Mbeya limeyafungia matawi sita ya Kanisa la Ufufuo na Uzima yaliyopo katika halmashauri sita za mkoa huo. Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Benjamin Kuzaga kufungiwa kwa matawi hayo kunatokana na tamko la serikali lililotolewa Juni 2, 2025 kupitia Msajili wa Jumuiya za kiraia nchini la kufunga …
MBEYA: JESHI la Polisi mkoani Mbeya limeyafungia matawi sita ya Kanisa la Ufufuo na Uzima yaliyopo katika halmashauri sita za mkoa huo.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Benjamin Kuzaga kufungiwa kwa matawi hayo kunatokana na tamko la serikali lililotolewa Juni 2, 2025 kupitia Msajili wa Jumuiya za kiraia nchini la kufunga makanisa ya Ufufuo na Uzima kutoendelea kutoa huduma katika matawi yake.
Kamanda Kuzaga amesema kuwa matawi ya Kanisa la Ufufuo na Uzima yaliyofungiwa ni pamoja na la lililopo ZZK katika Mamlaka ya Mji Mdogo wa Mbalizi Mbeya vijijini pamoja na lililopo mtaa wa Mnadani katika Mamlaka ya Mji Mdogo wa Rujewa wilayani Mbarali.
Mengine yaliyofungiwa ni yaliyopo katika Halmashauri za Wilaya za Chunya, Rungwe, Kyela pamoja na Halmashauri ya Jiji la Mbeya.