MAONI: Tanzania hata wajitanue vifua vipi, wakubali jina la nchi yao limechafuka

AJABU ya shingo kukataa kulala kitandani! Usiwaamini Watanzania wanapokwambia kuwa hawajali wala kubali kwamba nchi yao imechafuka jina kwa kukiuka haki za kibinadamu.
Wala usiwaamini wakitanua vifua na kudai hawaihitaji jamii ya kimataifa, eti mwonekano wao katika ngazi ya kimataifa si muhimu.
Taifa hilo linaihitaji jamii ya kimataifa kuliko jamii ya kimataifa inavyolihitaji.
Tumeshuhudia wiki nzima ya unoko na matusi ya kila aina kati ya Wakenya na Watanzania kutokana na kisa ambapo wanaharakati wa Kenya na Uganda waliteswa na kutupwa nje ya Tanzania.
Makachero wa Tanzania walimteka Bw Boniface Mwangi wa Kenya na Bi Agather Atuhaire wa Uganda, wakawadhulumu kwa namna ambavyo jamii isiyosoma wala kuendelea huwafanyia watu isiopenda.
Wawili hao walikuwa wamekwenda Tanzania kusikiliza kesi ya uhaini aliyosingiziwa mweyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Bw Tundu Lissu.
Kosa lake? Kuishinikiza serikali ifanye mabadiliko ya sheria ya uchaguzi ili uwe wa haki na wazi. Daima anayepinga juhudi za kuleta haki na uwazi ni mtuhumiwa wa kuwadhulumu watu.
Bila shaka si siri kwamba Tanzania, kwa sheria na mienendo, inaishi kama ilivyokuwa Kenya miaka ya sabini na themanini. Mateso dhidi ya mtu anayeshukiwa kuwa adui wa taifa yanashabikiwa na kushangiliwa na watu wanaojidhani wazalendo.
Ni nchi ya mafala na washamba pekee inayoona fahari na kushangilia wakati ambapo dola inakamua mapumbu ya wanaume na kuchomeka vijiti kwenye sehemu za siri za wanawake!
[caption id="attachment_173174" align="alignnone" width="2000"] Mwanaharakati wa Uganda Agather Atuhaire (kushoto) na mwenzake wa Kenya Boniface Mwangi wakisimulia mateso ya kushtua wanayosema walipitia wakiwa mikononi mwa maafisa wa usalama Tanzania. Picha|Evans Habil[/caption]
Ni nchi ya mafala na wazembe pekee ambayo bunge lake linasifu unyama huo na kutangaza nchi jirani adui, pasiwe na hata mbunge mmoja wa kupendekeza kuwe na ustaarabu, utu na maridhiano.
Haijalishi kwamba msimamo rasmi wa Serikali ya Kenya ni kuwa wanaharakati hao waliyataka wenyewe, hivyo wajutie makosa yao! Nchini Kenya wanakinukisha kweli; Serikali yetu inawachukia kwa kuwa inataka kukiuka haki zetu bila kukemewa na yeyote.
Ziara yao nchini Tanzania, ijapokuwa wameumizwa, ilifana sana. Nia kuu ilikuwa kuijulisha dunia kuhusu unyama wa serikali ya Tanzania dhidi ya Bw Lissu na kuifahamisha jamii ya kimataifa kuwa Tanzania ingali gizani, Sasa inanuka uvundo!
Puuza kelele na matusi yote unayosikia kutoka bunge la Tanzania. Hao wanaoruka juu na kufoka hawawezi kuunga moja na moja wakapata mbili, hawajui umuhimu wa jamii ya kimataifa wala diplomasia.
Wanaifanya kazi ya Rais Samia Suluhu Hassan, wanayedai kutetea, kuwa ngumu sana kwa kuwa, hata ikiwa atafaulu kumdhulumu Bw Lissu na kumzuia kuwania urais unaotarajiwa mwezi Oktoba, kazi ya kuitakasa nchi ni yake.
Anaelewa fika kina cha shimo alimoitoa Tanzania mara tu alipochukua hatamu za uongozi baada ya mtangulizi wake, John Magufuli, kufariki.
Magufuli alikuwa amekosana na karibu kila taifa muhimu duniani, hivyo kazi ya kwanza ya Bi Hassan ilikuwa kurejesha mahusiano kati ya Tanzania na jamii ya kimataifa.
Ili kufanikisha lengo hilo, alimteua mwanadiplomasia na msomi wa miaka mingi, Bi Liberata Mulamula, waziri wa Mambo ya Nje.
Aliitwa kutoka Chuo Kikuu cha George Washington, Amerika, ili kudhibiti hali kwa dharura.
Wakati huo Amerika ilikuwa imeikinai Tanzania si haba, hasa kutokana na jaribio la serikali kumuua Bw Lissu kwa kumfuma risasi 16 mwilini, miongoni mwa maovu mengine!
Bi Mulamula alitumika kwa muda mfupi, Tanzania ikakubalika tena, Rais Samia akaanza kupata mialiko ya kimataifa, kisha akageukia jambo jingine alilodhani la muhimu – kudhibiti mamlaka.
Bi Mulamula alifutwa kazi ghafla na Tanzania ikarejea kwenye shimo ilimoachwa na Magufuli. Unachoshuhudia wakati huu ni uovu, uzembe na jeuri ya nchi inayokimbia uwajibikaji wa kimataifa kisa na maana uchaguzi.
Ukiisha, na Bi Samia afanikiwe kubakia madarakani hata kwa kuikiuka Katiba ya nchi, utashuhudia akiwana kwa jino na ukucha katika juhudi za kujitakasa machoni pa jamii ya kimataifa.
Ili iache kabisa kukiuka haki za binadamu, Tanzania inapaswa kutengwa kwa kila namna na iwekewe vikwazo vikali. Ipewe masharti magumu ya kurejea kwenye jamii ya wastaarabu.
[email protected]