Hali ngumu ya uchumi yalazimu Wakenya zaidi kula matumbo badala ya nyama

Taifa Leo
Published: Jun 04, 2025 06:00:18 EAT   |  Business

WAKENYA wengi wamegeukia kula matumbo kama kitoweo kutokana na kupanda kwa gharama ya maisha. Hii ni kinaya kwani kwa muda mrefu nyama hiyo imekuwa ikichukuliwa kuwa ya watu wa kipato cha chini. Kulingana na Shirika la Kitaifa la Takwimu Kenya (KNBS), bei ya matumbo imepanda kwa karibu asilimia 34 katika kipindi cha miaka minne iliyopita, kutoka Sh260.46 kwa kilo mwaka wa 2020 hadi Sh344.92 mwaka wa 2024 kuashiria ongezeko kubwa la mahitaji. Kile ambacho hapo awali kilionekana kama bidhaa ya ziada isiyo na thamani sasa kimekuwa mbadala wa nyama kwa familia nyingi zinazopambana kumudu gharama ya maisha. “Nilipoanza, matumbo hayakuwa maarufu hivi,' anasema. "Sasa, nauza matumbo zaidi kuliko nyama ya kawaida. Watu hawawezi tena kumudu nyama ya ng’ombe," asema Bw Charles Wamugunda, muuzji bucha jijini Nairobi ambaye amekuwa kwenye biashara hiyo kwa zaidi ya miaka 10. Bw Wamugunda hupata matumbo kutoka vichinjio vya Kiserian na Dagoretti na anakiri kuwa hata bei ya jumla imepanda. “Bei inapopanda kule vichinjioni, sisi pia tunalazimika kuongeza. Kisha kuna ushuru ambao zamani hatukuwa tunalipa. Hii inaathiri faida,” anasema. Anaongeza, “Mazingira ya biashara pia yamebadilika, na ushuru wa ziada unapunguza kiwango cha faida. Kuna ushuru ambao siku hizi tunalazimika kulipa, tofauti na zamani.” Anasema wanaopendelea matumbo wameongezeka tofauti na zamani ambapo yalikuwa ya kawaida katika familia maskini. Katikati mwa jiji la Nairobi, Bw Dancan Kamau pia anashikilia maoni sawa na hayo. 'Miaka kumi iliyopita, nilikuwa ninauza matumbo kwa Sh150 kwa kilo. Leo hii, bei imeongezeka mara mbili,' anasema. 'Wateja wamehama kutoka nyama ya ng’ombe hadi matumbo. Ni nafuu na rahisi kupika.' Ingawa Bw Kamau hupata matumbo kutoka kwa mifugo wake mwenyewe, anasema faida imekuwa ndogo. “Gharama zimepanda kote, malisho hadi mishahara ya wafanyakazi. Hakuna faida kama zamani.” Hata hivyo, mahitaji ni makubwa. Katika siku nzuri, Bw Kamau huuza kati ya kilo 80 hadi 100 za matumbo. “Kwa mfano, kama baba alikuwa akinunua nyama ya ng’ombe kwa familia yake na sasa anapitia hali ngumu kifedha, atapendelea kubeba matumbo akirudi nyumbani kuliko kufika mikono mitupu. Wale waliokuwa wananunua nyama sasa wamehamia matumbo. Wakati wa hali ngumu, watu hubadilisha mambo,' aliongeza. Katika Kampuni Kenya Meat Commission (KMC), Meneja wa Mauzo na Masoko, Bi Lydia Mandila, alithibitisha kuhusu ongezeko la mahitaji. 'Tumeona ongezeko kubwa la mauzo ya matumbo, hasa katika maeneo ya watu wa kipato cha chini na cha kati,' anasema. "Ni nafuu na yana virutubisho." Bi Mandila anasema kuwa ingawa nyama ya ng’ombe bado ni bidhaa kuu ya KMC, matumbo yamekuwa bidhaa ya pili yenye faida ijapokuwa upatikanaji wake unategemea idadi ya ng’ombe wanaochinjwa. 'Katika kila kilo 130 za nyama ya ng’ombe, unapata takriban kilo 13 za matumbo,' anasema. 'Kwa hiyo kadri tunavyoongeza uchinjaji, ndivyo tunavyoweza kutoa matumbo zaidi.' Hata hivyo, anasema kuna msimu ambapo mauzo ya matumbo hupungua, hasa wakati wa sherehe ambapo watu hupendelea vipande bora vya nyama. 'Lakini kwa ujumla, tumerekodi mauzo na faida kubwa katika kipengele hicho. Hata tunafanya usambazaji unaolengwa, wakati mwingine hadi mitaa na maeneo ya kipato cha chini ili kufikia mahitaji,' aliambia Taifa Leo. "Kila mtu anakimbilia huko kwa sababu soko la Burma si kama zamani,' anasema.