Dk Jafo ataka sheria mpya aina ya biashara za wageni

Habari Leo
Published: Jun 06, 2025 12:31:39 EAT   |  Business

DAR ES SALAAM: WAZIRI wa Viwanda na Biashara, Dk Suleimani Jafo amesema ili kumaliza tatizo la wafanyabiashara wa kigeni kufanya biashara zinazofanywa na raia wazawa, ni muhimu kuunda sheria mpya ya wazi itakayobainisha aina ya biashara zinazopaswa kufanywa na raia wa kigeni. Dk Jafo amezungumza hayo leo Juni 6, 2025 jijini Dar es Salaam wakati …

DAR ES SALAAM: WAZIRI wa Viwanda na Biashara, Dk Suleimani Jafo amesema ili kumaliza tatizo la wafanyabiashara wa kigeni kufanya biashara zinazofanywa na raia wazawa, ni muhimu kuunda sheria mpya ya wazi itakayobainisha aina ya biashara zinazopaswa kufanywa na raia wa kigeni.

Dk Jafo amezungumza hayo leo Juni 6, 2025 jijini Dar es Salaam wakati akipokea ripoti ya timu iliyoundwa kukagua na kufuatilia wafanyabiashara wa kigeni waliopo Kariakoo ambao wanafuata sheria na kanuni za utoaji leseni na vibali vya kufanya kazi, kwa lengo la kuhakikisha fursa za wazawa zinabaki kwao.

Amefafanua kuwa tayari timu ya kundaa mapendekezo ya sheria hizo inaendelea mkoani Morogoro. Timu hiyo ilianza kazi Mei 5 hadi 30, 2025 iliundwa na jumla ya taasisi tano za serikali zinazohusika katika sekta ya biashara.

“Ili kumaliza tatizo hili, ni lazima tuwe na sheria itakayobainisha wazi mtu anayepaswa kufanya aina fulani ya biashara. Hivyo, hata kama sasa mtu anaonekana kuwa na haki ya kufanya biashara hiyo, mara tu sheria hiyo mpya itakapoanza kutumika, kibali chake kitaondolewa,”amesema.

Wadau wa fedha kidigitali wamlilia Dk Jafo

Aidha Dk Jafo amesema anaangilia uwezekano wa kuhakikisha mapendekezo hayo yanainigia kujadiliwa katika bunge linaondelea ili kupata ufumbuzi wa haraka zaidi.

“Kwa mujibu wa utaratibu, bunge hili ni la bajeti, na kwa sasa linashughulikia masuala ya bajeti pekee. Hata hivyo, tunatafuta njia ya kuwasilisha mapendekezo haya kwa hati ya dharura, au, ikishindikana, tuombe baadhi ya vifungu vya msingi viingizwe katika  Muswada wa Fedha (Finance Bill) kama hatua ya awali, kisha baadaye tukamilishe vifungu vilivyosalia,” ameongeza.

Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Dk Suleiman Serera, amesisitiza kuwa zoezi hili linapaswa kuwa endelevu na kufanyika mara kwa mara ili kuhakikisha tatizo hili linaondolewa kabisa.

Timu hiyo ya ukaguzi ilihusisha taasisi mbalimbali ikiwemo: Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Idara ya Uhamiaji, Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Idara ya Kazi, TANTRADE, TAKUKURU, BRELA, Tume ya Ushindani, Jumuiya ya Wafanyabiashara Kariakoo pamoja na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.

Timu hiyo ilifanya oparesheni yenye malengo ya, kubaini wafanyabiashara wa kigeni wanaofanya biashara bila vibali; Wanaokiuka sheria za kodi, wanaofanya biashara kinyume cha sheria za leseni, kufuatilia utekelezaji wa sheria za kazi,  kubaini kampuni zinazouza bidhaa chini ya viwango au bidhaa zilizopigwa marufuku, kubaini bidhaa bandia.

Akisoma ripoti hiyo, mwenyekiti wa timu hiyo, Thabit Massa amesema Jumla ya leseni  108 zilikaguliwa, leseni zilizotolewa na halmshauri ya jiji ni 40, 61 zilitolewa na BRELA, maduka 7 hayana leseni, ambazo zimeisha ni 9.

Tume ya ushindani ilikagua makampuni 53, maduka 9 yalikutwa na bidhaa bandia, TRA walikagua maduka 112, waliofika ofisi za TRA kwa ukaguzi 55, walioshindwa kufika ni 57 kwaajili ya ukaguzi, ambao walipewa barua za wito lakini hawakufika.

Waliopewa adhabu ya kodi ni 21, makusanyo ni milioni 34667, mabao wnaafanyiwa uchunguzi wa koodi ni 45.

Kwa Jeshi la Polisi ambao walijisajili kuangalia utaifa wao watu 183, wachina 135, Watanzania 32 ambao walibainika kutumika na wageni kufanya na biashara, Waingereza , Nigeria1, Kenya 5, Egypt 2, Orman 2, Wahindi 2, Dutch 1.

TBS ilikagua makampuni 83, walikokidhi sheria ya viwnago ni 70 waliokiuka 13, upande wa uhamiaji 151 walikaguliwa, wageni 12 waliondoshwa waliokuka taratibu za uhamiaji.