DC Lindi: Jitihada hazijawahi kumtupa mtu”

Habari Leo
Published: Jun 10, 2025 20:16:05 EAT   |  General

LINDI: Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Victoria Mwanziva, amewaahauri vijana wanaotoka wilaya hiyo kuongeza juhudi  kwa kila walifanyalo ili kutimiza ndoto zao. DC Mwanziva ametoa nasaha hiyo leo, Juni 10, 2025, wakati wa mahafali ya wanafunzi waliohitimu Mafunzo ya Ufundi Stadi Ngazi ya Tatu katika Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) kilichopo Lindi. Mkuu huyo wa …

LINDI: Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Victoria Mwanziva, amewaahauri vijana wanaotoka wilaya hiyo kuongeza juhudi  kwa kila walifanyalo ili kutimiza ndoto zao.

DC Mwanziva ametoa nasaha hiyo leo, Juni 10, 2025, wakati wa mahafali ya wanafunzi waliohitimu Mafunzo ya Ufundi Stadi Ngazi ya Tatu katika Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) kilichopo Lindi.

Mkuu huyo wa Wilaya ambaye alikuwa mgeni katika tukio hilo alisisitiza kwa vijana waliohitimu mafunzo na wale wanaoendelea na masomo katika chuo hicho kuweka jitihaha kwa kuwa hakuna njia ya mkato kufikia mafanikio.

Soma: PURA: Tumejaza gesi futi 301.33 miaka minne

“Wewe ambaye umepata ujuzi wako, nenda ukaweke jihitada utapata matokeo. Wewe ambaye bado unaendelea na masomo, nenda ukafanye jitihada utapata matokeo,” alisisitiza DC Mwanziva

Pamoja na nasaha hizo, Mkuu wa Wilaya amezipongeza Kampuni za mishati za Kimataifa za Equinor Tanzania na Shell Exploration and Production Tanzania Ltd kwa kufadhili vijana 24 kwa mwaka 2024/25 kutoka Mkoa wa Lindi kusoma kozi mbalimbali chuoni hapo.

Kupitia ufadhili wa kampuni hizo, vijana hao wameweza kusomea fani mbalimbali zikiwemo umeme, ubunifu wa mavazi na teknolojia ya nguo, uchomeleaji na uungaji vyuma, viyoyozi na majokofu, ufundi magari, na uashi.

Kampuni hizo pia zimewezesha vitendea kazi kwa wahitimu hao kwa lengo la kuwasaidia kutumia ujuzi walioupata kujiajiri.

Katika tukio hilo, DC Mwanziva aliwakabidhi wahitimu hao vitendea kazi hivyo mara baada ya kuwatunuku wahitimu vyeti.