Atwoli alalama kuwa ukuaji wa uchumi wa Kenya hauzalishi ajira

Taifa Leo
Published: Jun 05, 2025 05:55:08 EAT   |  Jobs and Career

KATIBU Mkuu wa Muungano wa Vyama vya Kutetea Masilahi ya Wafanyakazi (COTU) Francis Atwoli amelalamika kuwa licha ya uchumi wa Kenya kukua, mamilioni ya watu bado hawana ajira na maelfu ya wengine wamekimbilia sekta ya jua kali kujikimu kimaisha. Akihutubia kikao cha 113 cha Kongamano la Shirika la Kimataifa la Leba jijini Geneva, Uswizi Jumatano, Bw Atwoli alisema idadi kubwa ya vijana wasio na ajira Kenya ni tishio kwa taasisi za utawala zinazolaumiwa kwa kufeli kutoa nafasi bora za ajira na njia nyinginezo za kuwawezesha kuchuma mapato. “Nchini Kenya, sawa na katika nchi zingine zinazoendelea katika eneo la kusini mwa jangwa la Sahara, ukuaji wa kiuchumi haujazalisha nafasi za ajira. Zaidi ya watu milioni 5 hawana ajira na maelfu ya wengine wako katika sekta ya juakali. Asilimia 80 ya wasio na ajira wamekimbilia katika sekta hii,” Bw Atwoli akasema. Katibu huyo mkuu alisema ongezeko la idadi ya watu wasio na ajira limechochea idadi kubwa ya Wakenya kuelekea mataifa ya ng’ambo kusaka ajira. Idadi kubwa huelekea katika mataifa ya Ghuba, Uropa na Amerika Kaskazini, ambako alisema mazingira mabaya ya kufanyia kazi. “Malalamishi kuhusu ukiukaji wa haki za wafanyakazi yanaendelea kuripotiwa katika mataifa ya ng’ambo ambako Wakenya wanafanyakazi; haswa Uarabuni. Haya na mengine ndio shida ambazo Wakenya hupitia,” Bw Atwoli akaeleza. Kulingana na kiongozi huyo wa COTU, misukosuko ya kisiasa katika baadhi ya mataifa ya Kiarabu na vita ni changamoto zingine zinazowakumba Wakenya wanaofanya kazi ughaibuni. “Tangu Shirika la Kimataifa la Leba lilipobuniwa mnamo 1919, tumekuwa tukielekeza juhudi nyingi katika kuhakikisha kuwa ukuaji wa kiuchumi unazalisha nafasi za ajira zenye hadhi ambako haki za wafanyakazi zinalindwa,” Bw Atwoli akaeleza.